Kuna aina mbili za madawa zinazotumiwa ili kutoa mimba: mifepristone na misoprostol. Utoaji mimba kwa kutumia vidonge hufanya kazi vizuri ikiwa dawa hizi zote zinatumiwa kwa pamoja. Walakini, ikiwa mifepristone haipatikani, misoprostol pekee pia itafanya kazi ili kumaliza ujauzito na bado dawa hii ni salama.
Chagua ikiwa ungependa kujifunza juu ya maagizo ya utoaji mimba kwa njia salama kwa kutumia mifepristone na misoprostol au misoprostol pekee.
Kabla ya kuanza, soma ushauri wetu juu ya Kabla ya Kutumia Vidonge. Kuwa na uhakika:
Kwa kutoa mimba ukitumia mifepristone na misoprostol, utahitaji kuchukua kidonge vya 200mg vya mifepristone na vidonge vinne hadi vinane vya 200mcg vya misoprostol. Pia utahitaji kuwa na dawa ya kupunguza maumivu mkononi, kama ibuprofen ili kukusaidia kudhibiti maumivu. Dawa za Acetaminophen na paracetamol hazifanyi kazi kwa hayo maumivu wakati wa kutoa mimba kwa hivyo hazifai.
Hivi ndivyo mifepristone na misoprostol hutumiwa pamoja ili kumaliza ujauzito:
Meza kidonge chenye 200mg cha mifepristone ukitumia maji.
Subiri masaa 24 hadi48.
Weka vidonge 4 vya misoprostol (200 mcg kila moja) chini ya ulimi wako na vikae hapo kwa dakika 30 hadi viyeyuke. Hupaswi kuongea au kula kwa dakika hizi 30, kwa hivyo ni vizuri kukaa kimya mahali ambapo hautasumbuliwa Baada ya dakika 30, kunywa maji na kumeza kila kitu cha vidonge kilichobaki. Huu pia ni wakati mzuri wa kutumia dawa ya kupunguza maumivu kama ibuprofen kwa sababu maumivu ya ghafla yataanza.
Hapa, utaanza kutokwa na damu na maumivu ya ghafla katika masaa 3 baada ya kutumia vidonge 4 vya misoprostol.
Masaa 24 baada ya kutumia vidonge 4 vya misoprostol, kama haukuanza kutokwa na damu au hauna hakika kuwa utoaji mimba haukufaulu, weka vidonge 4 zaidi vya misoprostol chini ya ulimi wako. Acha zikae hapo kwa dakika 30 ili ziyeyuke. Baada ya dakika 30, kunywa maji na kumeza kila kitu cha vidonge kilichobaki.
Jifunze ni lipi unalotarajia baada ya kutumia mifepristone na misoprostol hapa.
Ikiwa utahisi maumivu ya ghafla, ibuprofen ni dawa nzuri ya kukabiliana na maumivu hayo. Unaweza nunua ibuprofen ya 200 mg zinazouzwa madukani (bila ruhusa ya daktari) katika nchi nyingi. Chukua vidonge 3 hadi 4 (200 mg kila moja) kila masaa 6 hadi 8. Ikiwa unahitaji kitu cha ziada kwa kupunguza maumivu, unaweza pia kutumia vidonge 2 vya Tylenol (325 mg) kila masaa 6 hadi 8.
Kama una wasiwasi juu ya mchakato wa utoaji mimba na ungependa msaada zaidi, unaweza kuwasiliana na marafiki wetu kwa www.safe2choose.org, www.womenhelp.org au www.womenonweb.org.
Kama ulitumia dawa za mifepristone na misoprostol ili utowe mimba, labda hauitaji kutembelea mtoa huduma ya afya kwa ziara ya kufuatilia unavyoendelea. Dawa hizi ni nzuri sana hivi kwamba Shirika la Afya Ulimwenguni linapendekeza kuwa unahitaji kufuatiliwa unavyoendelea ikiwa tu:
Kabla ya kuanza, soma ushauri wetu juu ya Kabla ya Kutumia Vidonge. Kuwa na uhakika:
Ikiwa mifepristone haipatikani katika mahala unapoishi, unaweza tumia misoprostol peke yake kwa kumaliza ujauzito.
Kwa kutoa mimba ukitumia misoprostol pekee, utahitaji kutumia vidonge kumi na mbili vya misoprostol 200mcg. Pia utahitaji kuwa ibuprofen ambayo ni dawa ya kudhibiti maumivu. Acetaminophen na paracetamol hazifanyi kazi ya kudhibiti maumivu wakati wa utoaji mimba, kwa hivyo hazifai.
Hivi ndivyo misoprostol peke yake hutumiwa kumaliza ujauzito:
Weka vidonge 4 vya misoprostol (200 mcg kila moja) chini ya ulimi wako na vikae hapo kwa dakika 30 hadi viyeyuke. Hupaswi kuongea au kula kwa dakika hizi 30, kwa hivyo ni vizuri kukaa kimya mahali ambapo hautasumbuliwa Baada ya dakika 30, kunywa maji na kumeza kila kitu cha vidonge kilichobaki. Huu pia ni wakati mzuri wa kutumia dawa ya kupunguza maumivu kama ibuprofen kwa sababu maumivu ya ghafla yataanza.
Subiri masaa 3.
Weka vidonge vingine 4 vya misoprostol (200mcg) chini ya ulimi wako na vikae hapo kwa dakika 30 hadi vitakapoyeyuka
Subiri masaa mengine 3.
Weka vidonge vingine 4 za misoprostol (200mcg) chini ya ulimi wako na vikae hapo kwa dakika 30 hadi vitakapoyeyuka.
Utakapotumia vidonge hivi, utaanza kutokwa na damu na kuwa na maumivu ya ghafla. Hakikisha umetumia vidonge vyote 12 hata kama utaanza kutokwa na damu kabla ya kumaliza vyote.
Jifunze ni lipi unalotarajia baada ya kutumia misoprostol hapa.
Ikiwa utahisi maumivu ya ghafla, ibuprofen ni dawa nzuri ya kukabiliana na maumivu hayo. Unaweza nunua ibuprofen ya 200 mg zinazouzwa madukani (bila ruhusa ya daktari) katika nchi nyingi. Chukua vidonge 3 hadi 4 (200 mg kila moja) kila masaa 6 hadi 8. Ikiwa unahitaji kitu cha ziada kwa kupunguza maumivu, unaweza pia kutumia vidonge 2 vya Tylenol (325 mg) kila masaa 6 hadi 8.
Kama una wasiwasi juu ya mchakato wa utoaji mimba na ungependa msaada zaidi, unaweza kuwasiliana na marafiki wetu kwa www.safe2choose.org, www.womenhelp.org au www.womenonweb.org.
Ikiwa umetumia misoprostol, labda hauitaji kutembelea mtoa huduma ya afya kwa ziara ya kufuatilia maendeleo yako. Dawa hizi ni nzuri sana hivi kwamba Shirika la Afya Ulimwenguni linapendekeza kuwa unahitaji kufuatiliwa unavyoendelea ikiwa tu:
Tovuti hii inaweza kuhitaji kuki zisizojulikana na huduma anuwai za mtu mwingine ili iweze kufanya kazi kunavyotakikana. Unaweza kusoma Sheria na Masharti yetu na Sera za Faragha . Ukitaka kuendelea kutumia tovuti hii, ni sharti utupe idhini ili uweze kufanya hivyo.