Kabla ya kutumia tembe

Hakikisha unajisikia vizuri kabisa na umejiandaa kabla hujatoa mimba kwa kutumia vidonge.

Mimba kikokotoleo (calculator)

Ujauzito wako ni wa muda gani? Utafiti unaonyesha kuwa mara nyingi utoaji mimba kwa kutumia vidonge unapendekezwa kwa mimba zenye umri chini ya wiki 13. Tumia kikokotoleo (calculator) hiki kujua ujauzito una muda gani?

Ikiwa kipindi chako cha mwisho kilianza tarehe au baadaye:

Bado unaweza kuzingatia utumiaji wa kidonge cha kutoa mimba

Vya Kuzingatia

Wakati unaposumbuliwa na IUD (KITANZI)

Kama umeweka kitanzi/lupu kwenye kizazi chako (kwa mfano coil au yenye homni ya progesterone) lazima kiondolewe.

Wakati ambapo unaishi na VVU

Kama wewe unaishi na maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU), hakikisha huumwi zaidi, unatumia dawa za kupunguza makali ya VVU na afya yako ni nzuri.

Kama unajali faragha yako

KKama unataka utoaji mimba wako uwe jambo la kibinafsi iwezekanavyo, weka kidonge cha kutoa mimba chini ya ulimi badala ya kukiweka katika sehemu za uke Iwapo kwa hali isiyotarajika una matatizo na kuhitaji ushauri wa daktari, tembe zinaweza kuonekana iwapo ulitumia kwa njia ya uke. Katika baadhi ya nchi, unaweza kushtakiwa tembe zinapopatikana katika uke wako.

Wakati unaponyonyesha

Kama unanyonyesha mtoto, dawa ya misoprostol inaweza kusababisha mtoto kuhara. Ili kuepuka hili, mnyonyeshe mtoto kwanza ndipo unywe dawa ya misoprostol halafu subiri masaa 4 kabla ya kumnyonyesha tena mtoto.

Wakati unaposumbuliwa na upungufu wa damu

Kiswahili; Iwapo una upungufu wa damu (una madini pungufu kwenye damu) wasiliana na mtoa huduma aliye umbali usiopita dakika thelathini anayeweza kukusaidia unapohitaji. Iwapo una upungufu wa damu uliokidhiri, pata ushauri wa daktari kabla ya kutumia tembe za kuavya mimba

Ushauri Wa Jumla

Kula chakula kidogo (kwa mfano vyakula vikavu au vya kukausha inaweza kukusaidia usipate kichefuchefu)

UKuwa na mtu mmoja ambaye ataweza kukupatia kama chai ya moto au kitu cha chakula na kukuangalia kama unapenda, inaweza ikasaidia.

Kunywa maji mengi kipindi chote cha mchakato huu

Inashauriwa kunywa tembe za ibuprofen kabla ya kuitumia misoprostol kusaidia kupunguza maumivu

Wakati matumizi ya tembe za misoprostol,hakikisha uko kwenye eneo ambapo una faragha k kwa mfano ama nyumba yako ambapo unaweza Kiswahili; kujilaza na kupumzika kwa masaa machache baada ya kutumia dawa.

Hakikisha umeweka tayari mpango wa usalama kabla ya kutumia tembe za kuavya mimba, hili ni la muhimu iwapo utahitaji msaada wa matibabu ya dharura

Kutengeneza mpango wa usalama

Kulingana na shirika la Marekani la uzazi na jinakolojia, uavyaji wa mimba iliyo miezi mitatu au chini kwa kutumia tembe ni mojawapo ya taratibu za tiba salama . Hata hivyo, unapaswa kutayarisha ipasavyo kwa matibabu ya dharura kama itakavyohitajika. Zingatia maswali yetu hapa chini ili kusaidia kutengeneza mpango wako wa usalama iwapo kama utakavyohitaji.

Kituo cha matibabu cha dharurua kilicho karibu na kinachofunguliwa masaa ishirini na manne(24hours) kiko wapi?

Unahitaji kuwa na uwezo wa kufika kwenye kituo nkwa saa 1 au chini. (Kama una upungufu wa damu, unapaswa kuwa na uwezo wa kufika huko kwenye kituo kwa dakika 30.)

Utafika vipi kwenye kituo chako cha matibabu ya dharura?

Je, kuna mtu atakayekuwa nawe na anayeweza kukufikisha kwa gari? Je, utachukua teksi? Utatumia Usafiri wa umma? Itagharimu pesa ngapi na je, inapatikana masaa ishirini na manne(24hours)? Kumbuka, sio salama kuendesha gari mwenyewe kwenda hospitalini wakati wa dharura ya matibabu.

Ni yapi utakayowaeleza wahudumu wa afya na madaktari?
  • Uavyaji wa mimba kutumia tembe una vikwazo vya kisheria nchini mwako? Ni nini utakachowaeleza wahudumu wa afya na madakatari ili waweze kuelewa msaada unaohitaji, huku ukilinda usalama na siri yako? Tuna baadhi ya mapendekezo iwapo unahitaji msaada wa taarifa na habari za kutoa inapohitajika.
  • Utakachowaambia wahudumu wa afya Katika baadhi ya nchi, kuavya mimba ukitumia tembe ni kinyume cha sheria. Hii ina maana kwambwa utakapohitaji msaada wa matibabu ya dharura, uwe mwangalifu unachosema. Kuavya mimba kw akutumia madawa kuna ishara sawa na mimba inayotoka kwa njia ya kawaida( pia hujulikana kama avyaji kwa hiari). Tumetayarisha baadhi ya majibu ambayo unaweza ukatumia:

Marejeo:

Tovuti hii inaweza kuhitaji kuki zisizojulikana na huduma anuwai za mtu mwingine ili iweze kufanya kazi kunavyotakikana. Unaweza kusoma Sheria na Masharti yetu na Sera za Faragha . Ukitaka kuendelea kutumia tovuti hii, ni sharti utupe idhini ili uweze kufanya hivyo.