Baada ya kutumia tembe

Kuna njia mbili za uaviaji mimba kwa utabibu. Njia zote ni bora kabisa:

Utajisikiaje baada ya kutumia vidonge vya kutoa mimba?

Baada ya kutumia tembe: Mifepristone

Unaweza kutokwa damu kidogo baada ya kumeza mifepristone. Hii ni kawaida!

Baada ya kutumia tembe: Misoprostol

Maumivu ya tumbo na kutokwa damu ndio matokeo makubwa. Dalili hizi ni nzuri kwa sababu inaonyesha kuwa dawa inafanya kazi. Lakini, ni kwa kiasi gani utapata maumivu ya tumbo na kutokwa na damu?

Kwa wanawake wengine, maumivu ya tumbo ni makali sana – zaidi kuliko maumivu wakati wa hedhi (kama unapata maumivu ya tumbo wakati wa hedhi).

Kwa wanawake wengine, hutokwa na damu nyingi kuliko inayotoka wakati wa hedhi. Pia ni kawaida kufuja damu masaa machache ya mwanzo baada ya kunywa misoprostol. Wingi wa damu utalingana na umri wa mimba.

Kwa wanawake wengine, maumivu ni kidogo na damu inayotoka sawa na ile ya wakati wa hedhi.

Usishtuke ukitokwa na damu zaidi kuliko hedhi ya kawaida. Hii ni kawaida.

Ukipata maumivu ya tumbo, dawa ya Ibuprofen ni dawa nzuri kupunguza maumivu. Unaweza kununua Ibuprofen ya milligram 200 bila ya karatasi ya dawa kutoka kwa daktari kwenye nchi nyingi. Kunywa vidonge 3-4 kila baada ya masaa 6-8. Hii itakusaidia kupunguza maumivu ya tumbo.

Unaweza Kula na kukunywa jinis unavyotaka

Jaribu kupumzika na kutulia mpaka utakapohisi nafuu

Wanawake wengi huhisi nafuu chini ya masaa ishirini na manne( 24)

Angalizo:

Wiki mbili baada ya kutoa mimba, vipimo vitaendelea kuonyesha kua bado una ujauzito hii inatokana na homoni zilizoko ndani ya mwili wako. Kama bado unahisi dalili za ujauzito (maumivu ya matiti, kichefuchefu, uchovu n.k) baada ya kutumia vidonge, muone daktari.

Kuwa mwangalivu?

Wakati mimba inavyotoka, dalili hap juu ni kawaida. Kuwa makini. Chini ni baadhi ya ishara kwamba unaweza kuwa katika hatari ya kupata matatizo makumbwa.

Iwapo utajaza vitamba viwili vya hedhi kwa masaa mawili mfululizo baada ya kudhania kwamba ushaavya mimba, hii ni ishara ya kufuja damu kwa wingi.

Unatakiwa kupata msaada wa kitabibu kama unatoka damu nyingi kiasi hiki. Kuloanisha pedi inamaanisha pedi kubwa yote imeloana damu mbele na nyuma, pembeni na pembeni na juu mpaka chini.

Maumivu Makali:

Kama unapata maumivu makali sana ambayo hayapungui hata baada ya kunywa dawa ya Ibuprofen, pata msaada wa kitabibu. Maumivu makali sana huenda ikamaanisha umepata matatizo makubwa ya mimba. Maumivu yasiyopungua ambayo hayapungui hata baada ya kunywa dawa ya Ibuprofen inaweza kuwa dalili ya hatari. Tunashauri mwanamke yeyote mwenye mimba nayepata maumivu atafute msaada wa kitabibu.

Unajisikia kuumwa sana?:

Unaweza kupata homa, kichefuchefu na kutapika siku ambayo umekunywa misoprostol ambayo ni kitu cha kawaida. Unatakiwa kujisikia nafuu zaidi kila siku baada ya kutumia vidonge vya kutoa mimba, na sio kuumwa. Kama utajisikia kuumwa Zaidi siku yoyote baada ya kumeza misoprostol unahitaji msaada wa kitabibu haraka.

Waandishi:

  • Yote yaliyomo kwenye wavuti hii yameandikwa na timu ya HowToUseAbortionPill.org kwa kufuata viwango na itifaki kutoka Shirikisho la Kitaifa la Utoaji Mimba, Ipas, Shirika la Afya Ulimwenguni, DKT Kimataifa na carafem.
  • Shirikisho la Kitaifa la Kutoa Mimba (NAF) ni chama cha kitaalam cha watoaji mimba huko Amerika ya Kaskazini, na kiongozi katika harakati za uchaguzi. Yaliyomo kwenye HowToUseAbortionPill.org inahusiana na Miongozo ya Sera ya Kliniki ya mwaka 2020 iliyotolewa na NAF.
  • Ipas ndio shirika pekee la kimataifa linalolenga tu kupanua ufikiaji wa utoaji salama wa mimba na uzazi wa mpango. Yaliyomo kwenye HowToUseAbortionPill.org inahusiana na Sasisho za Kliniki Katika Afya ya Uzazi 2019 iliyotolewa na Ipas
  • Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) ni wakala maalum wa Umoja wa Mataifa unaohusika na afya ya umma ya kimataifa. Yaliyomo kwenye HowToUseAbortionPill.org inahusiana na Utoaji mimba salama wa mwaka 2012: mwongozo wa kiufundi na sera kwa mifumo ya afya iliyotolewa na WHO.
  • DKT International ni shirika lisilo la faida lililosajiliwa mnamo mwaka 1989 ili kuzingatia nguvu ya uuzaji katika jamii katika baadhi ya nchi kubwa zilizo na mahitaji makubwa ya uzazi wa mpango, kinga ya VVU / UKIMWI na utoaji mimba salama.
  • carafem ni mtandao wa kliniki unaotoa utalaam wa kufaa wa utoaji mimba salama na uzazi wa mpango ili watu waweze kudhibiti idadi na nafasi ya watoto wao.

Marejeo:

Tovuti hii inaweza kuhitaji kuki zisizojulikana na huduma anuwai za mtu mwingine ili iweze kufanya kazi kunavyotakikana. Unaweza kusoma Sheria na Masharti yetu na Sera za Faragha . Ukitaka kuendelea kutumia tovuti hii, ni sharti utupe idhini ili uweze kufanya hivyo.