Nani Anaweza Kutumia Tembe za Kuavya Mimba?

Kama mimi ni mwanamke mnene (au mwenye uzani unaozidi), nahitaji kumeza tembe Zaidi?

La, tumia idadi sawa ya tembe tunazopendekeza kwa kila mtu. Tafiti zinaonyesha kuwa ufanisi wa dawa haupungui kwa wanawake wanene au wanaozidi uzani. Hauhitaji kumeza kipimo tofauti au kumeza tembe Zaidi.

Je ikiwa nimegundua kuwa nina mimba ya mapacha?

Hauhitaji kubadili kipimo au idadi ya tembe ikiwa umegundua kuwa una mimba ya mapacha. Utaratibu unaofanana ndio hutumika kwa wanawake wenye mimba za mapacha.

Je ikiwa nimewahi kutumia tembe ya kuavya mimba ufanisi wake unaweza kupungua?

La, kila mimba ni tukio la kipekee. Ikiwa uliwahi kutumia tembe ya kuavya mimba awali, hauhitaji kipimo zaidi ikiwa utaitumia tena kwa mimba tofauti isiyohitajika.

Ninaweza kumeza misoprostol nikiwa nimechopezwa IUD?

Ikiwa una kidude cha kuzuia mimba katika tumbo la uzazi (kama vile koili au IUD ya progesterone ), ni lazima ukitoe kabla ya matibabu ya kuavya mimba

Naweza kumeza misoprostol ninaponyonyesha?

Ikiwa unanyonyesha mtoto, tembe za misoprostol zinaweza kusababisha mtoto kuhara. Ili kuzuia hii, nyonyesha mtoto, meza tembe za misoprostol, kisha subiri saa 4 kabla ya kumnyonyesha tena.

Naweza kutumia tembe za kuavya mimba ikiwa nina HIV?

Ikiwa unaishi na HIV, hakikisha kuwa uko hali dhabiti, unatumia dawa za kupunguza makali ya virusi, na kuwa afya yako ni nzuri.

Naweza kumeza tembe ya kuavya mimba ikiwa nina anemia?

Kama una anemia (viwango vidogo vya madini katika damu yako), tambua mhudumu wa afya asiye zaidi ya dakika 30 mbali nawe ambaye anaweza kukusaidia ukiitaji msaada. Ikiwa umezidiwa na anemia, tafuta ushauri wa daktari kabla ya kutumia tembe ya kuavya mimba.

Je tembe ya kuavya mimba ni hatari ikiwa nilijifungua kwa upasuaji?

La, kutumia tembe za kuavya mimba mapema unapokuwa mja mzito ni salama hata kama ulijifungua kwa njia ya upasuaji.

Kama nitatumia tembe ya kuavya mimba na bado niwe na uja uzito baadaye, mtoto atakayezaliwa atakuwa na kasoro za kuzaliwa?

Hakuna uhusiano ambao umepatikana kati ya mifepristone na kasoro za kuzaliwa. Hata hivyo misoprostol huwa inasababisha kiwango kidogo cha ongezeko za kasoro za kuzaliwa. Kama utameza misoprostol na bado ungali mja mzito baada ya kumeza tembe, unaweza kupoteza mimba kwa njia ya kawaida. Ikiwa hautapoteza mimba hiyo na uwe nayo hadi wakati utimie, hatari ya kasoro za kuzaliwa huongezeka kwa 1% (mtoto mmoja kwa kila 100).

Awali nilifanyiwa ufungaji wa uzazi wa kike (ukataji mirija ya uzazi). Haikufanya kazi na nikawa mja mzito. Uja uzito ulikuwa katika mrija (uja uzito usio katika tumbo la uzazi). Sasa mimi ni mja mzito tena. Je ni salama kwangu kutumia tembe za kuavya mimba?

La, si salama kutumia tembe za kuavya mimba ikiwa unajua kuwa uko katika hatari ya kuwa na uja uzito usio katika tumbo la uzazi. Kwa sababu ulikatwa mirija ya uzazi, unajua kuna kovu katika mrija (futuza). Hiyo ndio maana labda uja uzito wako wa mwisho ulitokea nje ya tumbo la uzazi. Futuza ndipo yai la mwanamke linarutubishwa na mbegu za kiume. Uja uzito unaanza kukua na husafiri katika mrija hadi tumbo la uzazi. Ikiwa mrija wako una kovu, uja uzito wa awali unaweza ukanaswa katika mrija. Uja uzito unapokua, unaweza kusababisha mrija kupasuka. Ikiwa mrija utapasuka, hii inaweza kusababisha umwagikaji wa damu ndani yako, na ni tishio kwa maisha yako. Uko katika hatari ya kupata uja uzito mwingine nje ya tumbo la uzazi. Haustahili kutumia tembe za kuavya mimba hadi mhudumu wa afya ahakikishe kuwa uja uzito uko katika tumbo la uzazi na si katika mirija yako.

Naweza aje kuavya mimba ikiwa nimethibitishwa kuwa na uja uzito nje ya tumbo la uzazi?

Kwanza, unastahili kujua kuwa wanawake wengi hawawezi kujua wako katika hali hii hadi wafanyiwe kipimo cha idadi ya marudio ya mawimbi ya sauti. Uja uzito nje ya tumbo la uzazi hauwezi kudumu hivyo hata katika nchi ambapo uaviaji mimba ni kinyume cha sheria wanawake wanaweza kuwa na utaratibu wa kisheria kwa kutamatisha huu uja uzito.

Marejeo

Tovuti hii inaweza kuhitaji kuki zisizojulikana na huduma anuwai za mtu mwingine ili iweze kufanya kazi kunavyotakikana. Unaweza kusoma Sheria na Masharti yetu na Sera za Faragha . Ukitaka kuendelea kutumia tovuti hii, ni sharti utupe idhini ili uweze kufanya hivyo.